
Yafahamu mambo matatu yenye utata katika mswada wa fedha wa Kenya 2025
Dakika 5 zilizopita
Bajeti ya kitaifa nchini Kenya ya mwaka ujao wa kifedha (2025/2026) inatarajiwa kusomwa bungeni na Waziri wa fedha John Mbadi alhamisi Juni 12.
Lakini kabla wabunge hawajapata fursa ya kusikiliza na baadaye kujadili kuhusu makadirio yatakayokuwepo, Wakenya wanaendelea kutoa maoni yao kuhusu vipengee ambavyo wanahisi hawakubaliani navyo, hasa katika mswada wa fedha ambao huorodhesha kodi zitakazotozwa ili kufadhili bajeti inayopendekezwa ya Kes 4.356 trilioni ($33.6bn).
Taarifa za kuwafahamisha Wakenya kuhusu yanayopendekezwa katika mswada huo wa fedha zimeanza kuchapishwa katika mitandao ya kijamii huku wengi wakitumia X kueleza kero lao na mapendekezo, lakini pia kumekuwa na majukwaa rasmi ya umma yaliyoandaliwa na serikali ili kutoa maoni kwa mujibu wa sheria.
Mwaka huu serikali inafanya nini tofauti, ikizingatiwa kwamba Rais William Ruto alilazimika kufutilia mbali mswada wa fedha mwaka 2024 kutokana na maandamano ya vijana wa Gen Z?
Mwandishi wa BBC Peter Mwangangi anaangazia masuala matatu yenye utata.