
Makumi kwa maelfu ya waandamanaji wanatarajiwa siku ya Jumamosi kote Marekani, Canada, Mexico, na nchi za Ulaya kushutumu mageuzi makubwa yaliyotekelezwa tangu kurejea kwa Donald Trump katika Ikulu ya White House. Zaidi ya maandamano 1,200 yamepangwa katika ardhi ya Marekani.
Imechapishwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
Takriban maandamano 1,200 yamepangwa kote Marekani siku ya Jumamosi , Aprili 5, katika kile ambacho waandalizi wanasema itakuwa siku kubwa zaidi ya maandamano dhidi ya Rais Donald Trump na mshauri wake Elon Musk.
Tangu arejee katika Ikulu ya White House, Donald Trump amebadilisha kwa kiasi kikubwa sera ya Marekani ya mambo ya nje na ya ndani, na hivyo kusababisha ukosoaji kutoka kwa upinzani na waandamanaji wanaonuia kuingia mitaani kwa wingi kwa kauli mbiu “Hands Off!”.
Kulingana na Ezra Levin, mwanzilishi mwenza wa kundi la Indivisible, moja ya makundi yanayoandaa maandamano ya Jumamosi, lengo ni kuandaa “maandamano makubwa ambayo yanatuma ujumbe wazi kabisa kwa Musk, Trump, wabunge wa chama cha Republicans katika Baraza la Congress, na washirika wote wa MAGA (Make America Great Again): Hatutaki wachukue demokrasia yetu, jamii zetu, shule zetu, marafiki zetu na majirani zetu.”
Baadhi ya makundi ya wanaharakati 150 yamejiandikisha kushiriki katika maandamano hayo, kulingana na tovuti ya tukio hilo.