Wilaya ya Masasi mkoani Mtwara, imepiga marufuku usafirishaji wa wanafunzi wa shule za awali kwa kutumia bodaboda. Hatua hii imechukuliwa baada ya kubainika kuwepo kwa baadhi ya watoto wenye umri wa kuanzia miaka mitano walioanza kuathirika na matatizo ya afya likiwemo tatizo la nimonia inayohusishwa na matumizi ya usafiri huo.
Uamuzi huo unalenga kulinda afya na usalama wa watoto wadogo na kuhimiza wazazi kutumia njia salama zaidi za usafiri kwaajili ya watoto wao.
#azamnewsupdates
✍John Kasembe
Mhariri| @official_jennifersumi