WHO yanaonya juu ya kuongezeka mashambulio ya virusi vya mtandaoni dhidi ya hospitali

Shirika la Afya Duniani (WHO) na nchi hamsini zimeonya juu ya kuongezeka mashambulizi ya virusi vya kuombea vikombolea (ransomware) dhidi ya hospitali.

Hivi majuzi, wadukuzi kadhaa walishambulia data za kompyuta za watu binafsi, makampuni au taasisi mbalimbali kwa kutumia virusi wakitaka kupewa vikomboleo ili kuondoa virusi hivyo.

Tedros Adhanom Ghebreyesus, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani, ameliambia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwamba mashambulizi ya ransomware kwenye hospitali yamezidi na kuongezeka, na kusema: “Mashambulizi hayo kwenye hospitali ni suala la uhai na kifo.”

Tedros Adhanom amesisitiza umuhimu wa kuwepo ushirikiano wa kimataifa kwa ajili kukabiliana na mashambulizi hayo na kuongeza kuwa: Uhalifu wa mtandaoni, ikiwa ni pamoja na ransomware, ni tishio kubwa kwa usalama wa kimataifa.

Baraza la Usalama

Pia, zaidi ya nchi 50 zimetoa taarifa ya pamoja zikilaani nchi ambazo zinaruhusu mashambulizi hayo ya virusi vya kuombea kikomboleo (ransomware ) na kuonya kwamba, mashambulizi haya yanaweka maisha ya binadamu katika hatari na ni tishio dhidi ya usalama na amani ya kimataifa.