WHO yajibu tuhuma za US: Hatuegemei upande wa nchi yoyote mwanachama, tunazingatia sayansi

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani WHO Dkt. Tedros Adhanom Ghebreyesus amesisitiza kuwa shirika hilo haliegemei upande wa nchi yoyote mwanachama na kwamba limeanzishwa kwa ajili ya kuhudumia nchi zote na watu wote.