
Shirika la afya duniani limesema wataalam wake wanachunguza ugonjwa mpya usiojulikana nchini DRC baada ya mlipuko miwili tofauti kuripotiwa mapema mwaka huu.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
Kwa mujibu wa WHO eneo la Bolamba Magharibi wa wilaya ya Equateur limethibitisha visa vya watu 12 waliogonjeka ikiwemo vifo vya watu wanane mwezi Januari. Mapema mwezi huu, visa 158 na vifo 58 viliripotiwa katika eneo la Basankusu.
Wiki iliopita, watu 141 waligonjeka katika eneo la Basankusu. Hakuna vifo vilivyoripotiwa hadi tukichapisha ripoti hii.
Shirika la WHO linasema kupitia uchunguzi uliongezeka, watu 1,096 waligunduliwa kuambukizwa wakati wengine 60 wakithibitishwa kufariki katika eneo la Basankusu na Bolomba.
Dalili za ugonjwa huo ni pamoja na joto mwilini, kuumwa na kichwa, kutokwa na jasho, kuharisha, kukohoa, kutokwa na damu puani pamoja na kuumwa na misuli.
Nchi ya DRC inakabiliwa na milipuko mbalimbali ya magonjwa ikiwemo Ebola, Mpox kulingana na Shirika la afya duniani WHO.
Kikosi maalum cha wataalam wa afya ikiwemo wale wa WHO kimetumwa kuchunguza hali inavyoendelea.