Waziri wa ulinzi wa Uingereza amezuru Kenya

Waziri wa Ulinzi wa Uingereza, John Healey akiwa ziarani nchini Kenya, amekutana familia ya Agnes Wanjiru, ambaye alipatikana ameuawa mwaka 2012 na mwili wake kutupwa kwenye shimo la maji taka, baada ya kuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi na mwanajeshi wa Uingereza.

Imechapishwa:

Dakika 1

Matangazo ya kibiashara

Healey amekutana na mama yake, Agnes Wanjiru, baada ya família hiyo kwa miaka mingi, uchunguzi kuhusu mauaji ya mpendwa wao.

Wanjiru, ambaye wakati wa kifo chake alikuwa na umri wa miaka 21, inaripotiwa kuwa alikwenda kwenye maeneo ya burudani na mwanajeshi wa Uingereza, katika mji wa Nanyuki, kabla ya kupatikana ameuawa.

Waziri huyo wa ulinzi, kwenye ukurasa wake wa kijamii wa X, amesema Uingereza itaendelea kushirikiana na serikali ya Kenya, ili familia ya Wanjiru ipate haki.

Uingereza imekuwa ikishtumiwa kwa kupuuza mauaji hayo, baada ya kubainika kuwa, mwanajeshi huyo alikuwa katika kikosi cha BATUK ambacho kina kikosi cha kudumu mjini Nanyuki kwa ajili ya mazoezi.

Oktoba mwaka 2021, Gazeti la The Sunday Times, lilichapisha ripoti kuwa mwanajeshi wa Uingereza alikiri kwa wenzake kuwa alimuua Wanjiru na hata kuwaonesha mwili wake na ripoti hiyo iliwafikia wakuu wake, lakini hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa.

Kenya ilianzisha uchunguzi mwaka 2019 lakini ripoti ya kilichojiri, haijawahi kubainika, huku ucunguzi wa hadhari uliokuwa uanze mwaka 2024 ukiahirishwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *