Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Ridhiwani Kikwete, ametoa wito kwa j…

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Ridhiwani Kikwete, ametoa wito kwa j…

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Ridhiwani Kikwete, ametoa wito kwa jamii kupewa elimu zaidi kuhusu fursa za zabuni zinazotengwa kwa makundi maalum kupitia ununuzi wa umma.

Akizungumza katika kongamano la taasisi ya PPRA lililofanyika jijini Arusha Juni 16, 2025, Waziri Ridhiwani amesema Serikali imeweka msingi imara wa kuwawezesha vijana, wanawake na watu wenye ulemavu kushiriki kikamilifu katika uchumi wa nchi.

Ameeleza kuwa serikali imechukua hatua sita muhimu kuwawezesha makundi haya, ikiwemo agizo la kisheria la kutenga asilimia 30 ya zabuni zote za umma kwa ajili ya makundi maalum, hatua inayolenga kukuza uchumi jumuishi katika zama za mabadiliko ya kidigitali.

Waziri Ridhiwani amesema moja ya changamoto kubwa ni uelewa mdogo wa wananchi kuhusu uwepo wa fedha zinazotokana na ununuzi wa umma, hivyo ni muhimu kwa madiwani, wakurugenzi na viongozi wa serikali za mitaa kushirikishwa kikamilifu katika utoaji wa elimu hiyo.

Aidha, amesema jitihada hizo zimeanza kuonesha mafanikio, ambapo makundi maalum sasa yanajitokeza kwa wingi kunufaika na mikopo ya asilimia 10 inayotolewa na halmashauri kutoka kwenye mapato ya ndani.

✍ Mwandishi Wetu
Mhariri @claud_jm
#AzamTVUpdates

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *