Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Mipango na Uwekezaji), Profesa Kitila Mkumbo ametaja kuwa sekta ya sanaa na burudani imeongoza kw…

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Mipango na Uwekezaji), Profesa Kitila Mkumbo ametaja kuwa sekta ya sanaa na burudani imeongoza kw…

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Mipango na Uwekezaji), Profesa Kitila Mkumbo ametaja kuwa sekta ya sanaa na burudani imeongoza kwa kasi ya ukuaji kwa mwaka 2024, ikikua kwa kwa asilimia 17.1.

Ametaja sekta nyingine zilizofuata kwa ukuaji mkubwa ni sekta ya uzalishaji, sekta ya usafirishaji na usambazaji wa umeme iliyokuwa kwa kwa asilimia 15.4, huku habari na mawasiliano ikirekodi ukuaji wa asilimia 14.3. Aidha, sekta ya fedha na bima pamoja na sekta ya afya nazo zimeonyesha mwenendo chanya na kuchangia kuimarika kwa huduma za kijamii na miundombinu ya uchumi.

Pamoja na sekta hizo zinazokuwa kwa kasi, Prof. Mkumbo alibainisha kuwa kilimo, ujenzi na uchimbaji wa madini na mawe ndizo sekta tatu kuu zilizobeba karibu nusu ya ukuaji wa pato la taifa.

✍ @claud_jm
#AzamTVUpdates

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *