Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Mipango na Uwekezaji), Profesa Kitila Mkumbo amesema pato la Taifa la Tanzania kwa mwaka 2024 lil…

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Mipango na Uwekezaji), Profesa Kitila Mkumbo amesema pato la Taifa la Tanzania kwa mwaka 2024 lil…

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Mipango na Uwekezaji), Profesa Kitila Mkumbo amesema pato la Taifa la Tanzania kwa mwaka 2024 lilifikia shilingi trilioni 156.6, ikilinganishwa na trilioni 148.8 zilizorekodiwa mwaka 2023.

Hii ni sawa na ukuaji wa asilimia 5.5, jambo linaloifanya Tanzania kuingia kwenye orodha ya nchi zenye ukuaji mkubwa zaidi wa pato la taifa katika Ukanda wa Afrika Mashariki.

Amesema hayo bungeni leo alipokuwa akiwasilisha taarifa ya Hali ya Uchumi kwa mwaka 2024 na Mpango wa Maendeleo ya Taifa kwa mwaka 2025/26.

✍ @claud_jm
#AzamTVUpdates

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *