Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Prof

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Prof

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo, ameliambia Bunge kuwa kwa mujibu wa tathmini ya kitafiti iliyofanywa hivi karibuni na taasisi ya Afrobarometer, asilimia 71 ya wananchi wanaridhika na utendaji wa serikali na asilimia 70 wanasema nchi iko katika mwelekeo sahihi.

Akiwasilisha bungeni mpango wa hali ya uchumi wa Taifa kwa mwaka 2024 na mpango wa maendeleo wa Taifa kwa mwaka wa fedha 2025/2026, Prof. Mkumbo amesema kuwa wakati wastani wa kukubalika kwa serikali katika nchi nyingi za Afrika ni asilimia 40, Tanzania imepata asilimia 71, jambo linaloashiria kiwango cha juu cha imani ya wananchi kwa serikali yao.

#AzamTVUpdates
✍Alpha Jenipher
Mhariri | John Mbalamwezi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *