Waziri wa Mambo ya Nje wa Rwanda: ‘Umoja wa Mataifa sio Biblia’, tutaendelea kuzipinga ripoti zake

Waziri wa Mambo ya Nje wa Rwanda Olivier Nduhungirehe amesema, Umoja wa Mataifa sio Biblia, na kwamba nchi yake itapinga ripoti zake za madai kwamba Kigali inawaunga mkono waasi wa M23 wanaopigana na jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo mashariki mwa nchi hiyo.