Waziri wa Mambo ya Nje wa Afrika Kusini: Tunapinga kufurushwa Wapalestina, hatutasalimu amri mbele ya vitisho vya Trump

Waziri wa Mambo ya Nje wa Afrika Kusini, Ronald Lamola, amesema kuwa nchi za bara hilo zina msimamo mmoja juu ya haja ya kusuluhisha mgogoro wa Ukanda wa Gaza ndani ya suluhisho la mataifa mawili, akisisitiza kwamba Pretoria haitarudi nyuma kuhusiana na msimamo wake katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki.