Waziri wa Mafuta: Sera ya kusimamisha uuzaji mafuta ya Iran nje ya nchi imefeli na itaendelea kufeli

Waziri wa Mafuta wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Mohsen Paknejad amesema vikwazo havina tija yoyote na akasisitiza kwamba, sera ya kuufanya uuzaji mafuta ya Iran nje ya nchi ufikie kiwango cha sifuri imefeli na itaendelea kufeli.