Waziri wa Mafuta: Jamhuri ya Kiislamu ya Iran haina changamoto yoyote katika kuuza mafuta nje ya nchi

Waziri wa Mafuta wa Iran amesema kuwa Iran haina tatizo lolote katika uga wa kuuza na kusafirisha mafuta nje ya nchi.

Mohsen Paknejad ameyasema hayo akijibu swali lililoulizwa kwamba je baada ya kuingia madarakani Rais mpya wa Marekani Donald Trump bei na ubora wa mafuta yanayouzwa na Iran nje ya nchi itabadilika au la.

Ameeleza kuwa Wizara ya Mafuta ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, haina wasiwasi wowote katika uga wa kuuza na kusafirisha mafuta nje ya nchi.  

Waziri wa Mafuta wa Iran pia ameeleza kuwa wafanyakazi wenzake katika Idara ya Masuala ya Kimataifa ya wamejadili suala la  kuchukua hatua zinazohitajika kwa ajili ya kuuza mafuta ghafi nje ya nchi katika mazingira yoyote.

“Iran itaendelea kuuza na kusafirisha mafuta nje ya nchi bila ya changamoto yoyote,” amesisitiza waziri Mohsen Paknejad.