WAZIRI RIDHIWANI AIPONGEZA BENKI YA CRDB KUWEZESHA VIJANA KIUCHUMI

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Ridhiwani Kikwete akizungumza wakati wa hafla ya wanahisa wa benki ya CRDB iliyofanyika katika viwanja vya kituo cha kimataifa cha mikutano cha Arusha (AICC)  jijini Arusha.

Na Mwandishi Wetu – Arusha

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Ridhiwani Kikwete, amepongeza jitihada zinazofanywa na Benki ya CRDB katika kuwawezesha vijana kiuchumi ili wajiletee maendeleo na taifa kwa ujumla.

Mhe. Ridhiwani ametoa pongezi hizo wakati wa hafla maalumu ya chakula cha jioni kwa Wanahisa iliyoandaliwa na benki hiyo ambayo imefanyika katika viwanja vya kituo cha kimataifa cha mikutano cha Arusha (AICC), tarehe 17 Mei, 2025 jijini Arusha.

Aidha, amesema kupitia programu ya IMBEJU ambayo inalenga kuwanufaisha vijana na wanawake imekuwa chachu ya maendeleo kwa vijana kwa kutoa fursa za mitaji, mafunzo, mitandao ya kibiashara na kuwaunganisha na fursa za kimataifa.

“Taasisi za fedha nchini zimekuwa bunifu katika kuhakikisha makundi mbalimbali kwenye jamii ikiwemo vijana na Watu wenye Ulemavu wanashirikishwa kikamilifu katika uchumi kupitia huduma zinazowagusa moja kwa moja,” amesema

Amesema, Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan itaendelea kuweka mazingira wezeshi ya Uwekezaji nchini kwa ajili ya kuchochea ajira na kuwezesha vijana kiuchumi.

Kadhalika, Mhe. Ridhiwani Kikwete amepongeza Bodi ya Wakurugenzi, menejimenti na wafanyakazi wa benki hiyo kwa juhudu na ubunifu wanaoonyesha katika kuhudumia jamii.

Maadhimisho miaka 30 ya Benki ya CRDB pamoja Semina ya Wanahisa wa Benki hiyo yalifunguliwa rasmi na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango tarehe 16 Mei 2025 katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC).

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Ridhiwani Kikwete akizungumza wakati wa hafla ya wanahisa wa benki ya CRDB iliyofanyika katika viwanja vya kituo cha kimataifa cha mikutano cha Arusha (AICC)  jijini Arusha.

Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB, Prof. Neema Mori (katikati) akieleza jambo katika hafla ya chakula cha jioni iliyoandaliwa na benki hiyo ambayo imefanyika katika viwanja vya kituo cha kimataifa cha mikutano cha Arusha (AICC),  jijini Arusha.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela akieleza jambo wakati wa hafla ya chakula cha jioni iliyoandaliwa na benki hiyo ambayo imefanyika katika viwanja vya kituo cha kimataifa cha mikutano cha Arusha (AICC) jijini Arusha.

Baadhi ya washiriki wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Ridhiwani Kikwete (hayupo pichani) wakati akizungumza katika hafla ya wanahisa wa benki ya CRDB iliyofanyika katika viwanja vya kituo cha kimataifa cha mikutano cha Arusha (AICC)  jijini Arusha.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Ridhiwani Kikwete akiteta jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela (kushoto) pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB Foundation, TullyEster Mwambapa (katikati) wakati wa hafla ya chakula cha jioni iliyoandaliwa na benki hiyo ambayo imefanyika katika viwanja vya kituo cha kimataifa cha mikutano cha Arusha (AICC),  jijini Arusha.

The post WAZIRI RIDHIWANI AIPONGEZA BENKI YA CRDB KUWEZESHA VIJANA KIUCHUMI appeared first on Mzalendo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *