Waziri Mkuu wa Uhispania: Sitaruhusu mpango wa Trump wa kuwafukuza Wapalestina huko Gaza

Waziri Mkuu wa Uhispania, Pedro Sánchez, amepinga vikali mpango wa Rais wa Marekani wa kutwaa Ukanda wa Gaza na kuwahamisha kwa nguvu Wapalestina hadi nchi jirani kama Jordan na Misri, akisisitiza kwamba Madrid haitaruhusu mpango huo kutekelezwa.