Waziri Mkuu wa Italia: EU isichukue msimamo unaogongana na wa Marekani katika kadhia ya Ukraine

Waziri Mkuu wa Italia Giorgia Meloni amesema, Umoja wa Ulaya haupaswi kuchukua msimamo ambao utakinzana na sera ya Marekani kuhusu Ukraine. Hayo ni kwa mujibu wa shirika rasmi la habari la Italia ANSA.