Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema Serikali itaendelea kuwalinda na kuwawezesha watu wenye ulemavu, wakiwemo wenye ualbino kwa…

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema Serikali itaendelea kuwalinda na kuwawezesha watu wenye ulemavu, wakiwemo wenye ualbino kwa…

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema Serikali itaendelea kuwalinda na kuwawezesha watu wenye ulemavu, wakiwemo wenye ualbino kwa kuhakikisha wanapata fursa stahiki za kiuchumi na kijamii.

Akihutubia kilele cha maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Uelewa Kuhusu Ualbino, yaliyofanyika leo Juni 13, 2025 katika Uwanja wa Mwanga Centre mkoani Kigoma, Majaliwa amesema Serikali imeendelea kuchukua hatua mahsusi kuimarisha ustawi na utoaji wa huduma muhimu kwa watu wenye ualbino, ikiwa ni pamoja na kutambua kundi hilo, kuimarisha sera na mifumo ya huduma.

Katika kuhakikisha watu wenye ulemavu wanawezeshwa kiuchumi, Waziri Mkuu amesema kuwa hadi Machi 2025, kiasi cha shilingi bilioni 5.48 kimetolewa kwa vikundi 891 vya watu wenye ulemavu kupitia mikopo ya halmashauri inayotokana na mapato ya ndani.

Aidha, alieleza kuwa ruzuku kwa vyama vya watu wenye ulemavu imeongezeka hadi kufikia shilingi milioni 230 kwa mwaka wa fedha 2024/2025, ikilinganishwa na milioni 200 zilizotolewa mwaka uliotangulia.

Kuhusu afya, Majaliwa amesema Serikali kupitia Bohari Kuu ya Dawa (MSD) imetumia zaidi ya shilingi milioni 500 kati ya Julai 2021 na Juni 2024 kusambaza mafuta maalum ya kuzuia saratani ya ngozi kwa watu wenye ualbino katika mikoa yote 26 ya Tanzania.

✍ Mwandishi Wetu
Mhariri @claud_jm
#AzamTVUpdates

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *