Wazayuni wazidi “kumkalia kooni” nduli wa Ghaza

Matokeo ya uchunguzi wa karibuni kabisa wa maoni uliofanywa na Kanali ya 12 ya televisheni ya Israel yanaonesha kuwa, walowezi wengi wa Kizayuni wanaoishi katika ardhi za Palestina zilizopachikwa jina bandia la Israel, wanachukizwa sana na kuendelea Benjamin Netanyahu kung’ang’ania kuwa waziri mkuu wa utawala huo.