“Wazayuni, kizingiti cha kupatikana uthabiti katika umma wa Kiislamu”

Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Amani na Usalama ya Kimataifa ya Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema utawala wa Kizayuni ndicho kikwazo kikuu cha kupatikana uthabiti na maendeleo endelevu katika ulimwengu wa Kiislamu na eneo la Asia Magharibi.