Bukoba. Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa Kagera imewafikisha mahakamani wafanyabiashara watano wauzaji na wazalishaji vinywaji vikali wilayani Karagwe.
Watano hao wamefunguliwa kesi mbili zenye mashtaka tisa yanayohusisha kuendesha viwanda bandia bila Leseni ambavyo vinatumika kuzalisha bidhaa hizo na kuuza bila kuwa stika zilidhibitishwa na TRA.
Washtakiwa hao wamefikishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Bukoba, Mkoa wa Kagera na gari (Cruiser la TRA) chini ya ulinzi mkali wa jeshi la Polisi.

Watuhumiwa wanaodaiwa kufanya biashara vinywaji vikali wilayani Karagwe wakiwasili katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Bukoba mkoa Kagera.
Wamefikishwa mahakamani hapo leo Jumatatu, Machi 24,2025 na kufunguliwa kesi mbili zenye mashtaka tisa ya uhujumu uchumi kwa kukutwa wanatengeneza na kuuza bidhaa za pombe kali bila vigezo pamoja kutokuwa na leseni.
Washtakiwa hao baada ya kufikishwa mahakamani hapo waliingizwa katika chumba cha mahakama kwa ajili ya kesi kutajwa na kusikilizwa na baada ya hapo wakili wa Serikali, Judith Mwakyusa kwa upande wa jamhuri akataja kuwa kesi ya kwanza namba 7238/2025 ya uhujumu uchumi inawakabili Mwesiga Reopard Rupia, Nelius Kaizilege Mwami, Julieth Ishengoma Kisheni, Herieth Deodatus Gervas na Mlokozi Egbert Emely.
Aidha wakili Judith amewasomea washtakiwa wote wanne mashtaka tisa yanayowakabili ambayo wanatuhumiwa kuyatekeleza kati Desemba, 2025 hadi Machi 2025.
Baada ya utaratibu wa kimahakama kuwasomea mashtaka hayo washtakiwa hao naye Hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama ya hakimu mkazi Bukoba, Janeth Masesa akawauliza washtakiwa kama wanakili kutenda makosa hayo, washtakiwa wote kwa pamoja wamekana makosa.
“Mshtakiwa namba moja hadi nne, mnakili kutenda kosa hilo?” washtakiwa kwa pamoja wakajibu hapana” aliuliza Hakimu Masesa.
Baada ya hatua hiyo kwa upande wa mawakili wawili wa utetezi wanaowawakilisha washtakiwa hao wanne mahakamani ambao ni Projestus Mulokozi pamoja na Frank Karoly wameomba dhamana na kisha washtakiwa wakadhaminiwa kwa masharti ya kimahakama.
Hata hivyo, kesi hiyo yakwanza ya uhujumu uchumi inayowakabili washtakiwa hao wanne imepigwa Karenda ya kusikilizwa na Hakimu Masesa, hadi Aprili 8, 2025 itakapoitwa tena.
Kwenye kesi ya pili ambayo ni namba 7243/2025 imefunguliwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA. Mkoa Kagera ya uhujumu uchumi ni kwa mfanyabiashara wa pombe kali katika Wilaya ya Karagwe, Mlokozi Egbert Emely.

Baadhi ya watuhumiwa wanaodaiwa kufanya biashara vinywaji vikali wilayani Karagwe wakiwa ndani ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Bukoba mkoa Kagera.
Kesi hiyo nayo imesikilizwa jana Machi 24, 2025 katika chumba cha mficho cha usikilizwaji cha mahakama chini ya hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama hiyo, Eliapokea Wilisoni.
Katika usikilizwaji wa kesi hiyo, Wakili wa Serikali kwa upande wa Jamhuri, Alex Giryago amemsomea mshatakiwa huyo namba tano mashtaka nane yote yakihusishwa suala la uhujumu uchumi kwa kutengeneza pombe kali na kusamba bila kufuata taratibu za TRA.
Mshtakiwa Mlokozi Egbert Emely akiwa na wakili wake anayemtetea Frank Karoly baada ya kusomewa mashtaka hayo mshtakiwa amekana kutotenda makosa hayo mbele ya Hakimu Wilsoni.
Wakili Karoly kwa upande wa utetezi katika shauri hilo, ameomba dhamana ya mteja wake na kukubaliwa kisha kesi hiyo kuahirishwa mpaka Aprili 2, 2025 itakapoitwa tena kwa ajili ya kusikilizwa.
Wakili wa Serikali kwa upande wa Jamhuri, Alex Giryago katika kesi ya kwanza 7238/2025 akiwasomea mashtaka tisa yanayowakabili watuhumiwa wanne hukusu makosa waliyotenda kati ya Desemba 2024 hadi Machi 2025.
Amesema mshtakiwa wa kwanza, wa pili na tatu wanakabiliwa na shtaka la kukutwa na bidhaa zisizolipiwa ushuru wa bidhaa na ambazo hazijapewa msamaha.
Wakili Alex, amesema shtaka la pili la Kutengeneza bidhaa zinazolipiwa ushuru bila ya kuwa na leseni linawakabili mshtakiwa namba moja na mbili, shtaka namba tatu ni kushindwa kuomba kibali cha kutengeneza bidhaa zenye ushuru kwa ajili ya eneo la utengenezaji na utunzaji linawakabili washtakiwa namba moja hadi tatu.
Na mashtaka mengine ni kushindwa kuwasilisha marejeo/ritani ya bidhaa zenye ushuru zilizozalishwa linamkabili mshatkiwa namba moja hadi mbili, shtaka namba tano ni kushindwa kutunza kumbukumbu ya stempu za kielektroniki pia linamkabili mshatkiwa namba moja na mbili.
Shtaka la kushindwa kubandika stempu za kielektroniki kwenye vifungashio vya bidhaa zinazolipiwa ushuru linamkabili mstakiwa namba moja na mbili kwenye kesi hiyo katika shtaka namba saba la kushindwa kulipa kodi Sh10.58 milioni linamkabili mshtakiwa namba moja peke yake.
Mashtaka mawili la nane na tisa katika kesi ya kwanza yanawakabili washtakiwa wa kwanza na wapili ambapo ni kusaidia ukwepaji kodi ya ushuru wa bidhaa na shtaka la mwisho ni kuisababishia hasara TRA kiasi cha Sh10.58 milioni ni kwa mshtakiwa namba moja na mbili.
Kwenye kesi namba mbili ambayo ni namba 7243/2025 ambayo pia ni kuhusu uhujumu uchumi inamkabili mshtakiwa namba tano ambaye ni Mlokozi Egbert Emely ambayo inajumuisha mashta nane yote yakifanana na yawashtakiwa wanne wakwanza waliyotanguliwa kusikilizwa.