Chuo Cha Uhasibu Arusha IAA kupitia Mradi wa HEET wamehitimisha Mafunzo ya siku tatu ya kujenga uelewa wa mradi huo kwa watumishi wa ajira mpya kada za Taaluma na Utawala yaliyofanyika katika Jengo la Ofisi ya Atomic Energy Commission Njiro jijini Arusha
Akifunga mafunzo hayo Mkuu wa Kitivo cha Biashara IAA Dkt. Martin Dome ameushukuru uongozi wa Chuo Pamoja na Mradi wa HEET kwa kufanikisha mafunzo hayo ambayo yatawawezesha watumishi hao wapya kupata muongozo wa utendaji kazi wao huku wakizingatia maalidi
Dkt.Dome amewataka watumishi hao kuyatumia vyema mafunzo na kuhakikisha wanakuwa wazalendo, watunzaji wazuri wa nyaraka za serikali, Pamoja na kuzingatia mifumo ya sheria zinazowaongoza wakiwa kazini
“Hakikisheni mnaenda kufanya kazi kwa kuzingatia maadili kwani itakuwa nyenzo muhumu na itapekekea kuipa sifa nzuri taasisi kutokana na ubora mtakaouonyesha mkiwa mnatekeleza majukumu yenu” amesema Dkt. Dome
Nae Afisa Takukuru Mkoa wa Arusha Gipson Isaya amesema utumishi wa umma ni dhamana hivyo amewahasa watumishi hao kuhakikisha wanaisaidia serikali kutoa huduma kwa wananchi bila la kujihusisha na masuala ya rushwa kwani ni hatari kwao na kwa taifa kwa ujumla
Chrispina Ntanga Mkufunzi msaidizi IAA kampasi ya Dar es salaam ni moja ya watumishi walioshiriki mafunzo, amesema elimu aliyoipata inaenda kumsaidia kufanya kazi kwa kuzingatia maadili Pamoja na kuendelea kupinga suala la rushwa kama mtumishi wa umma
Mafunzo haya yamefanyika kwa siku tatu na kuhudhuriwa na wadau kutoka taasisi mbalimbali waliohusika kutoa mafunzo, na mwisho washiriki ambao ni watumishi wapya IAA wamekula kiapo cha uadilifu kwa watumishi wa umma.
The post WATUMISHI WAPYA IAA WAASWA KUWA WAZALENDO NA KUZINGATIA MAADILI KAZINI appeared first on Mzalendo.