Watu wenye silaha wavamia kituo pekee cha afya katika jimbo la Upper Nile

Nchini Sudan Kusini, kituo pekee cha afya kinachomilikiwa na Madaktari wasiokuwa na mipaka MSF katika jimbo lenye mzozo la Upper Nile, kimefungwa baada ya watu wenye silaha kukishambulia.

Imechapishwa:

Dakika 1

Matangazo ya kibiashara

Kiongozi wa MSF nchini Sudan Kusini Zakariya Mwatia, amesema kwa sababu ya kuongezeka kwa matukio ya utovu wa usalama kwenye jimbo hilo, huduma zimesitishwa.

Mwatia amesema watu wenye silaha walivamia kituo hicho cha afya, wakati wagonjwa zaidi ya 100 walipokuwa wanapokea huduma mbalimbali za afya.

Licha ya wafanyakazi wa MSF kutojeruhiwa katika shambulio hilo, MSF inasema imelazimika kufunga kituo hicho kwa kuhofia usalama wa wafanyakazi wake na wagonjwa.

Kufungwa kwa kituo hicho, kinahatarisha maisha ya magonjwa katika jimbo la upper Nile hasa kipindi hiki, baada ya Shirika la UNICEF kuripoti kuwa maambukizi ya kipindupindu zaidi ya 40,000 kuripotiwa tangu mwezi Septemba mwaka uliopita.

Mapigano yaliyozuka mwezi Februari kati ya wanajeshi wa serikali na waasi wa White Army, wanaoaminiwa kumuunga mkono Makamu wa kwanza wa rais Riek Machar, ambaye amezuiwa nyumbani baada ya kukamatwa yanatishia kurejesha nchi hiyo kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *