
Takriban watu 36 wameuawa shahidi katika mashambulizi ya anga ya utawala wa Kizayuni katika mji wa kihistoria na kitamaduni wa Palmyra nchini Syria.
Duru ya kijeshi ya Syria imetangaza kuwa adui Mzayuni jana adhuhuri alitekeleza mashambulizi ya anga dhidi ya majengo kadhaa katika mji huo wa kihistoria na kujeruhi watu 50. Ndege za kivita za utawala wa Kizayuni zimetekeleza mashambulizi hayo katika mji wa Palmyra zikitokea katika kambi ya kijeshi ya Marekani huko al Tanf.
Katika miaka ya hivi karibuni, utawala wa Kizayuni umekuwa ukishambulia mara kwa mara mji mkuu wa Syria, Damascus na maeneo mengine ya nchi hiyo.
Unatawala wa Kizayuni unaofanya mauaji ya kimbari unatekeleza hujuma za kijeshi dhidi ya ardhi ya Syria katika hali ambayo mji mkuu wa nchi hiyo Damascus umeshambuliwa mara kadhaa na utawala huo ambapo Syria imelaani chokochoko hizo za Israel dhidi yake.
Syria imetuma barua kwa Umoja wa Matiafa na Baraza la Usalama ikilaani mashambulizi ya Israel dhidi ya ardhi ya nchi hiyo.