
Wapiganaji wenye silaha kutoka kundi la M23, ambalo limechukua udhibiti wa Goma, mji muhimu mashariki mwa DRC, wamewafukuza maelfu ya watu wanaowaona kuwa wahamiaji haramu kutoka Rwanda siku ya Jumamosi, shirika la habari la AFP limeripoti.
Imechapishwa:
Dakika 2 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Siku ya Jumatatu, msemaji wa jeshi la kundi hilo, Willy Ngoma, aliwasilisha kwa vyombo vya habari katika uwanja mkuu wa Goma wanaume 181 waliowataja kuwa ” raia wa Rwanda” wanaoishi nchini hump kinyume cha sheria.
Wanaume wote waliowasilishwa walikuwa na vitambulisho kiraia vya vya DRC, ambavyo M23 walivitaja kuwa vya uongo. Mwandishi wa habari wa shirika la habari la AFP ameripoti kwamba kundi hilo la wasi wa M23 kwa jumla lilichoma nyaraka hizo kwenye uwanja wa michezo.
Mamia kadhaa ya wanawake na watoto, ndugu za wale waliokamatwa, walijiunga nao kwenye uwanja wa ndege ndani ya malori yaliyokodiwa na M23.
Mmoja wa watu waliokamatwa, aliyejitambulisha kwa jina la Eric, aliliambia shirika la habari la AFP siku ya Jumatatu kwamba anatoka katika mji wa Karenga, ulioko Kivu Kaskazini, unaochukuliwa kuwa ngome ya kundi la Democratic Forces for the Liberation of Rwanda (FDLR).
FDLR ni kundi lenye silaha lililoanzishwa na viongozi wa zamani wa Kihutu wa Rwanda wa mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 dhidi ya Watutsi.
Mapema siku ya Jumamosi, watu 360 walipakiwa kwenye mabasi kutoka Goma, Eujin Byun, msemaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), ameliambia shirika la habari la AFP.
UNHCR ilibainisha kuwa “kurejeshwa kwa wakimbizi katika nchi zao za asili lazima kuwe salama, kwa hiari na kutekelezwa kwa heshima, kwa mujibu wa sheria za kimataifa.”
Msafara huo ulivuka mpaka hadi Rubavu magharibi mwa Rwanda, mwandishi wa AFP ameripoti.
“Tutafanya kila linalowezekana kuwaunganisha tena katika jamii, ili wawe na majukumu na haki sawa na Wanyarwanda wengine,” Prosper Mulindwa, meya wa wilaya ya Rubavu, amewaambia waandishi wa habari.
M23 na Kigali wanaishutumu Kinshasa kwa kuunga mkono FDLR na wamehalalisha mashambulizi yao mashariki mwa DRC kwa haja ya kuliangamiza kundi hili.
Familia nyingi zilizofurushwa na M23 zinatoka Karenga na zilizuiwa kurejea huko baada ya M23 kuchukua Goma, kulingana na vyanzo vya usalama na kibinadamu.
Familia hizo zilikuwa zikiishi katika kituo cha mapokezi cha watu waliokimbia makazi yao huko Sake, takriban kilomita 20 kutoka Goma, vyanzo vimesema.
Mwezi Machi, washukiwa 20 wa wapiganaji wa FDLR, waliokuwa wamevalia sare za majeshi ya Kongo, walikabidhiwa na M23 kwa mamlaka ya Rwanda.
Kinshasa ilishutumu tukio hilo na kusema ni “uzushi mbaya” unaolenga kudhalilisha jeshi lake.