
Wakaazi wa Walikale-centre wameanza kurejea hatua kwa hatua katika mji huo, ambao uko chini ya udhibiti wa waasi wa M23 tangu siku ya Jumatano, Machi 19, baada ya mapigano makali, Radio OKAPI inaripoti ikinukuu mashahidi.
Imechapishwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
Wakati wa Walikale-centre walikuwa wamekimbia mapigano kati ya jeshi la Kongo na waasi wa M23, wakiungwa mkono na jeshi la Rwanda.
Hali bado ni ya wasiwasi katika barbara kutoka Walikale-centre- kwenda Lubutu, ambapo mapigano yanaendelea kati ya pande husika.
Wakati huo huo, raia wanashtumu uporaji wa kimfumo unaofanywa na watu wenye silaha walnaovalia sare za kijeshi katika vijiji na miji kadhaa ya eneo hilo, haswa katika vitongoji vya Mubi, Ndjingala, Logu, Biruwe, Makana na Kangama, hadi mpaka kati ya mkoa wa Kivu Kaskazini na mkoa wa Maniema kulingana na Radio OKAPI.
Kulingana na mashahidi, uporaji huo ni wa kiwango kikubwa: mifugo, bidhaa, maduka na vitu vya kibinafsi vimechukuliwa.
Hali hii inasababisha hofu kutanda katika eneo hilo. Kutokana na hali hii, wakazi wa vijiji kadhaa wanapendelea kukimbilia mbali na barabara kuu na kuweka mali zao mbali kabisa ili kuepuka uporaji.
Vyanzo vya habari vya ndani vinaripoti kuwa timu za misaada ya kibinadamu zinaendelea na shughuli zao katika mji huo kwa kutambua waliojeruhiwa na kuchukuwa miili ya watu waliofariki, katika juhudi za kuzuia kuzuka kwa magonjwa ya milipuko.