Watu 54 wauawa na 158 wajeruhiwa katika shambulio la kijeshi sokoni huko Omdurman nchini Sudan

Idadi ya watu waliouawa kutokana na kushambuliwa kwa makombora na wapiganaji wa Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF) siku ya Jumamosi kwenye soko lenye watu wengi huko Omdurman, kaskazini mwa mji mkuu wa Sudan Khartoum, imeongezeka na kukfikia 54.