
Watu 50 wamepoteza maisha na wengine mamia hawajapatikana, baada ya boti waliyokuwa wanasafiria, kuzama kwenye ziwa Congo baada ya kushika moto, Kaskazini Magharibu mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Imechapishwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
Ripoti zinasema ajali hii ilitokea Jumanne usiku, baada ya boti hiyo iliyotengenezwa kwa mbao, na iliyokuwa na abiria karibu 400, kuzama karibu na mji wa Mbandaka.
Maafisa wanasema, abiria walioabiri boti hiyo, walikuwa wametoka katika mji wa bandari wa Matankumu kwenda Wilayanni Bolomba, wakati ajali hiyo ilipotokea.
Msako wa abiria wengine unaendelea, baada ya manusura wengine karibu 100 kuokolewa wakiwa hai na kupelekwa hospitalini, baada ya kujeruhiwa na kwa moto.
Moto ndani ya boti hiyo ulisababishwa na kitendo cha mwanamke mmoja, ambaye alikuwa ni abiria, kuamua kupika ndani ya boti hiyo, huku baadhi ya abiria, wakiwemo watoto na wanawake, wakitumbua majini na kupoteza maisha kwa kusundwa kuongelea.
Ajali za majini, hutokea sana nchini DRC kutokana na hali mbaya ya boti za kusafiria, ambazo hupakia abiria kupita kiasi.