Watu 44 wauawa katika shambulio la waasi wa SPLM-N huko Kordofan Kusini

Maafisa wa Sudan wametangaza kuwa watu wasiopungua 44 wameuawa na 28 kujeruhiwa katika shambulio lililotekelezwa na waasi wa harakati ya SPLM-N inayoongozwa na Abdelaziz al Hilu katika makao makuu ya jimbo la Korofan Kusini kusini mwa Sudan.