
Watu wasiopungua 23 wameuawa na watu wenye silaha katika mashambulizi manee tofauti, katika jimbo la Benue, kaikati mwa Nigeria, afisaa mmoja wa shirika la Msalaba Mwekundu amliambia shirika la habari la AFP siku ya Jumapili Mei 11, 2025.
Imechapishwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
Mashambulizi hayo yalitokoea jioni ya Mei 10 katika viji vinne. Mapigano huzuka mara kwa mara kati ya wafugaji na wakulima, kila upande ukitaka kuchukua udhibiti wa sehemu ya ardhi katikati mwa Nigeria.
Wafugaji wengi ni kutoka katika jamii ya Waislamu wa Fulani na wakulima wengi walikuwa Wakristo. Makabiliano hayo huchukuwa mara nyingi sura ya kidini au kikabila. Baadhi ya mashambulizi haya yalitokea katika maeneo ambayo tayari yalilengwa na mashambulizi mwezi mmoja uliyopita, ambayo yaligharimu maisha ya watu 56.
Watu wanane waliuawa katika kijiji cha Ukum, tisa katika kijiji cha Logo na watatu katika vijiji vya Guma na Kwande
Mashambulizi mawili yaliyotekelezwa na watu wenye silaha ambao hawajajulikana mwanzoni mwa mwezi Aprili katika jimbo jirani la Plateau yaligharimu maisha ya watu mia moja.