Watoto nchini Sudan Kusini wanafariki kutokana na kipindupindu

Watoto nchini Sudan Kusini wanakufa kutokana na ugonjwa wa Kipindupindu wakati huu pia wakitembea umbali mrefu kuvifikia vituo vya afya ambavyo hata hivyo vimefungwa baada ya Marekani kusitisha misaada ya nje, limeonya shirika la umoja wa mataifa.

Imechapishwa:

Dakika 1

Matangazo ya kibiashara

Kulingana na UNICEF, watoto nchini humo wanalazimika kutembea kwa muda mrefu ilikufikia maeneo ya matibabu ambayo hata hivyo yamefungwa baada ya Marekani kusitisha ufadhili wake katika sekta muhimu ya afya.

Aidha wasiwasi wa hali kuwa mbaya zaidi imebuliwa kutokana na mvutano wa sasa wa kiusalama kati ya rais Kiir na makamu wake wa Riek Machar, hali ambayo inatishia kulitumbukiza taifa hilo katika mapigano mengine ya wenyewe kwe wenyewe.

Tangu mwezi Septemba mwaka wa 2024, karibia visa Elfu arobaini vya maambukizo ya kipindupindu vimeripotiwa nchini humo kulingana na takwimu za UNICEF.

Nalo shirika la Save the Children limethibitisha kutokea kwa vifo vya watoto karibia watano ambao walikuwa wakielekea kutafuta matibabu mashariki mwa jimbo la Jonglei.

Save the Children imesema tayari imelazimika kufunga kliniki zake saba kati ya 27 baada ya kukosekana kwa ufadhili ambapo 20 zilizosalia zinakabiliwa na changamoto ya kifedha.

Limelazimika pia kupunguza idadi ya wafanyikazi wake nchini kote. Rais wa Marekani Donald Trump alitangaza kukatiza bajeti yake kwa shirika la misaada la Marekani USAID ambalo limekuwa la msaada mkubwa zaidi kwa mataifa mengi tu duniani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *