Watoto milioni 138 walishiriki ajira za utotoni 2024

Idadi hiyo inajumuisha karibu watoto milioni 54 ambao wanafanya ajira ambazo huenda zikaathiri afya na usalama wao.

Ripoti hiyo inasema visa vya ajira kwa watoto vinafanyika aghalabu katika kilimo huku mataifa yaliyo chini ya Jangwa la Sahara yakiathirika pakubwa ambapo watoto milioni 87 wanaathirika.

Watoto nchini Syria wakifanya kilimo
Watoto nchini Syria wakifanya kilimoPicha: VWPics/Imago

Idadi hiyo lakini inaonyesha kupungua kwa idadi ya watoto wanaoathirika na kwani katika kipindi cha kati ya mwaka 2021-2024 idadi ni watoto 138 walioshiriki ajira za watoto ikilinganishwa na mwaka 2016-2020 ambapo watoto milioni 160 waligundulika kufanya ajira.

Licha ya kupungua kwa idadi hiyo, lengo la kuangamiza ajira kwa watoto kufikia mwaka 2025 halitofikiwa kama ilivyoainishwa kwenye malengo ya Ustawi ya Umoja wa Mataifa.

Ripoti hii imetolewa kuelekea Siku ya Kimataifa ya Kupinga Ajira kwa Watoto Duniani itakayoadhimishwa Alhamis.

“Ripoti mpya ya ajira kwa watoto inaonyesha ukweli mchungu kwamba mamilioni ya watoto bado wananyimwa haki ya kusoma, kucheza na kuwa watoto, licha ya maendeleo yaliyopatikana,” alisema mkuu wa UNICEF Ujerumani, Christian Schneider.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *