Waterforce TZ na ndoto ya kuifanya Tanzania kuwa kinara uvumbuzi wa matibabu ya maji

Dar es Salaam. Usimamizi wa maji taka ni muhimu ili kupunguza athari kubwa za mabadiliko ya tabianchi, hata hivyo, nchini Tanzania, sekta hiyo inakabiliwa na uwezo mdogo wa kitaasisi, uratibu duni na kukosa washirika sahihi kuhudumia maji taka.

Katika suala hili, Waterforce Tanzania, ambayo ni mtoa huduma kamili za masuluhisho ya matibabu ya maji iko tayari kukushika mkono kama mshirika wa kuaminika kutatua changamoto zako.

Waterforce, siyo tu hutoa huduma za matibabu ya maji taka kwa kutumia mbinu bora za kisekta bali pia hujengea uwezo taasisi au jamii kumiliki miradi yao wenyewe kwa lengo la uendelevu.

Mtambo wa Matibabu ya Maji Taka wa kilo lita 120 ambao una teknolojia ya MBBR uliofungwa katika Kampuni ya Khetia Drapers Ltd.

Katika mahojiano maalumu na Gazeti la Mwananchi, Mkurugenzi Mtendaji wa Waterforce Tanzania, Shivanand Poojari ameelezea kuhu¬su maji taka, tasnia nzima ya matibabu ya maji na utendaji wa kampuni hiyo, tukiwa tunaadhimisha Siku ya Maji Duniani. Mazungumzo hayo yalikuwa kama ifuatavyo:

Swali: Kwa maslahi mapana ya wale ambao hawajui, unawezaje kuyatibu maji taka? Kuna athari gani za kiafya ikiwa maji hayatatibiwa vizuri?

Poojari: Vyanzo vikuu vya maji ghafi ni mvua, mito, maziwa, visi¬ma na bahari. Maji hutolewa kutoka kwenye vyanzo hivi na kutumika kwa majumbani na viwandani.

Baada ya matumizi au tuseme uzalishaji, maji taka hutolewa, ambayo lazima yatibiwe na kurudi kwenye chanzo chake ili kudumisha usawa wa kiikolojia na maelewano ya asili.

Matibabu ya maji taka hujumui¬sha hatua kadhaa za kuondoa uchafu kabla ya kurudishwa kwa usalama kwenye mazingira au kutumika tena.

Mchakato huo kwa kawaida ni pamoja na:

i. Matibabu ya msingi – Kuon¬doa taka ngumu kubwa na mashapo.

ii. Matibabu ya pili – Kutumia michakato ya kibayolojia ili kugawanya vitu vya kikaboni.

iii. Matibabu ya hali ya juu zaidi – Uchujaji wa hali ya juu na matibabu ya kemikali ili kuon¬doa vichafuzi vilivyosalia.

Ikiwa maji taka hayatatibiwa ipas¬avyo, yanaweza kuchafua vyanzo vya asili vya maji, kuathiri viumbe vya majini, kueneza magonjwa yanayo¬tokana na maji, na kuharibu ubora wa udongo, na hatimaye kuathiri afya ya umma na mazingira.

Swali: Kutokana na ongezeko la uzalishaji unaotumia maji kwa win¬gi, matibabu ya ongezeko la kiasi cha maji taka huleta changamoto kubwa. Je, ni ngumu kiasi gani kutibu maji taka katika hali kama hii?

Poojari: Changamoto ya matiba¬bu ya maji taka ya viwandani iko katika ugumu wa uchafuzi wenyewe, pamoja na metali nzito, kemikali, na mizigo yenye kiwango¬ kikubwa cha kaboni.

Mchakato wa matibabu unahitaji masuluhisho yaliyobuniwa mahsusi kwa ajili ya sekta husika-iwe sekta ya usindikaji wa chakula, dawa, nguo, madini, sukari, viwanda vya bia, n.k.

Teknolojia ya hali ya juu, wafanya¬kazi wenye ujuzi, na uwekezaji wa kifedha ni muhimu ili kushughulikia hali hiyo kwa ufanisi.

Kwa bahati mbaya, nchini Tanza¬nia, sekta hii bado inakabiliwa na ukosefu wa utaalamu wa kiufundi, uelewa, na sera sahihi za kudhibiti matibabu ya maji taka ya viwandani kwa ufanisi.

Swali: Kaya maskini ni wahanga wakubwa wa matatizo yanayohu-siana na maji taka na zina aidha uwezo mdogo au hazimudu kabisa gharama za masuluhisho hayo. Je, mnahakikishaje jamii hizo zinafikiwa na huduma hizo?

Poojari: Utaratibu wetu ni kubuni masuluhisho ya bei nafuu na ende¬levu yaliyolenga jamii zenye kipa¬to cha chini. Tunafanikisha hili kwa kufanya yafuatayo:

i. Kutoa mafunzo kwa jamii ili ziweze kujenga na kusimamia masuluhisho ya maji taka yali¬yogatuliwa. Badala ya kufun¬gua matawi mengi, tunazin¬gatia kuwawezesha watu bin¬afsi kuanzisha biashara katika maeneo yao husika.

ii. Kubuni teknolojia za ghara¬ma nafuu, zisizohitaji maten¬genezo ya mara kwa mara zin¬azofaa maeneo ya vijijini.

iii. Kushirikiana na Serikali za mitaa na mashirika yasiyo ya kiserikali kuanzisha mifumo midogo midogo ya kutibu maji taka katika maeneo ambayo hayajahudumiwa.

Mtambo wa Matibabu ya Maji Taka wa lita 100,000 kwa saa wenye teknolojia ya hali ya juu ya uchujaji maji uliofungwa katika Kampuni ya Sayona Fruits Ltd, kampuni tanzu ya Motisun Holdings Group.

iv. Kuhimiza ushirikiano kati ya sekta ya umma na sekta bin¬afsi ili kuhakikisha maji safi yanawafikia watu wote.

Tunaamini kwamba elimu ni muhimu, na tunaendelea kuende¬sha kampeni za uhamasishaji ili kuwasaidia watu kuelewa umuhimu wa usimamizi wa maji taka ili kulinda afya ya umma.

Swali: Ni aina gani ya huduma za matibabu ya maji taka mnazotoa zinazoendana na mahitaji ya Tanzania?

Poojari: Huduma zetu zinaendana na mazingira halisi ya Kitanzania. Huduma hizo ni:

i. Matibabu ya Maji Taka ya Viwandani – Haya ni masu¬luhisho maalumu kwa viwan¬da na mitambo ya utengene¬zaji.

ii. Matibabu ya Maji Taka ya Manispaa – Hii ni mitambo mikubwa ya kutibu maji taka kwenye jamii za mijini na viji¬jini.

iii. Mifumo ya Matibabu Iliyogat¬uliwa – Haya ni masuluhisho madogo madogo kwa kaya na biashara ndogo ndogo.

iv. Teknolojia ya Matibabu ya Maji Taka na Matumizi Mapya – Hii husaidia viwanda na jamii kupunguza upotevu wa maji.

v. Mafunzo na Kujenga Uwezo – Kuwawezesha wataalamu wa ndani kusimamia mifumo ya matibabu ya maji kwa ufanisi.

Lengo letu lipo kwenye masu¬luhisho yaliyobuniwa kwa ajili ya mazingira halisi, endelevu, na ya gharama nafuu ili kukidhi mahitaji mahususi ya Tanzania.

Swali: Je, ni miradi mingapi ya kuti¬bu maji taka imetekelezwa chini ya kampuni yako?

Poojari: Kwa miaka mingi, tume¬fanikiwa kukamilisha miradi mingi katika sekta tofauti, ikijumuisha:

i. Viwanda vya kutibu maji taka kwa tasnia mbalimbali.

ii. Miradi ya maji ya manispaa ya kutibu maji taka mijini na vijijini.

iii. Masuluhisho yaliyobuni¬wa kwa watu/taasisi binafsi kwenye biashara na makazi.

iv. Ushirikiano na mamlaka za mitaa kuboresha miundom¬binu ya maji taka.

Baadhi ya miradi inayofahamika ni pamoja na:

i. Motison Holding Group – Tumebuni na kusimika mtam¬bo wa kutibu maji taka wa Kilo lita 1200 ili kusindika taka kutoka kwenye utamu asilia wa matunda na kuyarejesha maji katika mzunguko wa matumizi.

ii. Sea Cliff Resort and Spa, Zan¬zibar – Tumefunga mfumo wa MBBR (10,000 lita kwa saa) wa uchakataji kwa ajili ya maji taka yanayozalishwa mahote¬lini.

iii. Kiwanda cha Sukari Zanzibar – Tumefanikiwa kusanifu na kufunga mtambo wa kutibu maji taka wa kilo lita 250 – USABR kwa ajili ya kiwanda kizima.

Tunaendelea kukuza mchango wetu, kuhakikisha jamii nyingi zin-apata maji safi na masuluhisho bora ya usimamizi wa maji taka.

Swali: Ni kinawazuia kufikia malen¬go yenu kama kampuni?

Poojari: Changamoto kubwa tunazokabiliana nazo ni pamoja na:

i. Vikwazo vya kisheria- Mam¬laka ya mapato na mamlaka nyingine za udhibiti mara nyingi hazifahamu kwa undani namna sekta yetu ina¬vyofanya kazi, shauku yetu ni waweze kutufahamu na hatimaye jambo hilo linaweza kuchangia maendeleo ya kitai¬fa na kusaidia biashara yetu kukua.

ii. Ukosefu wa Wafanyakazi Wenye Ujuzi – Sekta ya mat¬ibabu ya maji nchini haina wataalamu wa kutosha. Suala hili linachochewa na utitiri watu wasio na weledi katika sekta ya matibabu ya maji, ambao hawahamishi ujuzi kwa wenyeji.

iii. Rasilimali Chache za Kifedha – Benki zinasita kusaidia miradi ya matibabu ya maji kwa saba¬bu ya ukosefu wa ufahamu wa mtindo wa biashara hiyo.

iv. Kukithiri kwa Miundo ya Biashara – Biashara nyingi huzingatia kuagiza mifumo iliyotengenezwa tayari badala ya kuwekeza katika ukuzaji wa ujuzi wa ndani na uvumbuzi wa kiteknolojia.

Licha ya vikwazo hivi, tunaende¬lea kusonga mbele kwa kutoa mafun¬zo kwa watu, kuelimisha watunga sera, na kuhamasisha watu wengine kusaidia sekta hiyo.

Swali: Je, mipango yenu ya siku zijazo ikoje?

Poojari: Ndiyo, tuna mipango kabambe kadhaa ikiwamo:

i. Kupanua programu zetu za mafunzo ili kujenga nguvu kazi ya ndani yenye nguvu katika teknolojia ya kutibu maji.

ii. Kubuni masuluhisho ya kisasa ya kutibu maji taka kulingana na mahitaji ya Tanzania.

iii. Kushirikiana na Serikali na taasisi za fedha kuunda sera zinazosaidia sekta ya matiba¬bu ya maji.

iv. Kuongeza uelewa wa umma juu ya matibabu ya maji taka na athari zake kwa afya na mazingira.

v. Kuhimiza matumizi endelevu ya maji kupitia mipango ya kuchakata maji na kutumia tena.

Maono yetu ya muda mrefu ni kuo¬na Tanzania inakuwa kinara katika uvumbuzi wa matibabu ya maji, yenye masuluhisho yaliyobuniwa mahsusi nchini ambayo yananufais¬ha viwanda na jamii.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *