Watanzania wameshauriwa kutumia muda wao wa ziada baada ya kazi rasmi kwa shughuli za kujiongezea kipato badala ya kutumia muda …

Watanzania wameshauriwa kutumia muda wao wa ziada baada ya kazi rasmi kwa shughuli za kujiongezea kipato badala ya kutumia muda …

Watanzania wameshauriwa kutumia muda wao wa ziada baada ya kazi rasmi kwa shughuli za kujiongezea kipato badala ya kutumia muda huo kulalamika au kulaumu mazingira.

Mshauri na Mtaalamu wa Masuala ya Kifedha, Charles Ligonja, ametoa wito huo alipokuwa akizungumza katika kipindi cha Hallo Wikiendi kinachorushwa na UTV. Amesema kuwa kuna fursa nyingi zinazopatikana baada ya muda wa kazi ambazo zinaweza kutumika kwa shughuli halali na zenye manufaa. Amebainisha kuwa mabadiliko ya hali ya maisha yanategemea juhudi binafsi na si kusubiri msaada wa nje.

#AzamTVUpdates
✍Nifa Omary
Mhariri | John Mbalamwezi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *