Watanzania kushirikishwa mageuzi ya teknolojia

Watanzania kushirikishwa mageuzi ya teknolojia

Dar es Salaam. Ili kuendana na mageuzi ya teknolojia hasa ya vifaa vya kisasa vya kielektroniki wadau sekta hiyo wamewahakikishia Watanzania kwa kutoa bidhaa salama, zenye ubora wa hali ya juu na ubunifu wa kisasa.

Katika kuhakikisha hilo kampuni ya utengenezaji wa vifaa vya umeme wa majumbani ya Hisense imezindua rasmi luninga ya kisasa yenye ukubwa wa inchi 116 ikiwa ni kubwa zaidi kuwahi kuzinduliwa katika ukanda wa Afrika, sambamba na jokofu la milango miwili lenye teknolojia bora.

Hafla ya uzinduzi huo imefanyika jijini Dar es Salaam leo Alhamisi Mei 21, 2025 huku ikihudhuriwa na wadau wakuu wa sekta ya vifaa vya kielektroniki pamoja na burudani mbalimbali.

Rais wa Hisense kwa Ukanda wa Mashariki ya Kati na India, Jason Ou amesema Hisense imejikita katika kurahisisha maisha ya Watanzania kwa kutoa bidhaa salama, zenye ubora wa hali ya juu na ubunifu wa kisasa.

“Tunaelewa mahitaji ya Watanzania, na dhamira yetu ni kufika sokoni na kushughulikia mahitaji hayo kama chapa inayokua kwa kasi zaidi. Kupitia bidhaa zetu, tumejizatiti kuboresha ustawi wa jamii na kuchangia ukuaji wa uchumi wa Taifa,” amesema Ou.

Mtendaji Mkuu wa Mars Communication, Tahera Kareem amesema dhamira ya kampuni yao ya kuhakikisha bidhaa bora zinapatikana kwa Watanzania na kwa bei nafuu.

“Furaha huanzia nyumbani. Ndiyo maana tunaleta bidhaa bora zinazotambulika kimataifa kwa bei nafuu ili kumwezesha kila Mtanzania kufurahia maisha bora,” amesema muda mfupi kabla ya kusaini tena mkataba wa kuwa msambazaji rasmi wa Hisense nchini, hatua ya kuendeleza ushirikiano wa kuunganisha Watanzania na bidhaa bora.

Tangu mwaka 2019, Mars Communication imekuwa msambazaji pekee wa Hisense nchini Tanzania. Kareem amesema Hisense haiwaachi nyuma Watanzania katika mageuzi ya kiteknolojia, bali inaendelea kuleta furaha, amani na matumaini kwa familia nyingi nchini kupitia bidhaa zake.

Kwa upande wake, Vivi Liu, Makamu wa Rais wa Hisense kwa Ukanda wa Mashariki ya Kati na Afrika na Meneja Mkuu wa Hisense Afrika Kusini, amesema nafasi ya Hisense katika kubadilisha maisha ya watu kote barani Afrika si kwa bidhaa zake bora pekee, bali pia kwa kutoa ajira na kukuza ujuzi wa watu katika jamii mbalimbali.

Aidha, Mkurugenzi wa Mauzo ya Nje, Grant Pendlebury amesema bidhaa mpya zilizozinduliwa zimetengenezwa kwa teknolojia ya kisasa, zikiwa na uwezo mkubwa wa kuokoa nishati na kudumu kwa muda mrefu zikiwa tayari kwa soko la ndani na kimataifa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *