Wataalamu, watafiti na watunga sera kutoka nchi mbalimbali duniani wapo jijini Arusha kushiriki katika mkutano wa kutathmini ute…

Wataalamu, watafiti na watunga sera kutoka nchi mbalimbali duniani wapo jijini Arusha kushiriki katika mkutano wa kutathmini ute…

Wataalamu, watafiti na watunga sera kutoka nchi mbalimbali duniani wapo jijini Arusha kushiriki katika mkutano wa kutathmini utekelezaji wa sera madhubuti za kupambana na umaskini kupitia malengo ya maendeleo endelevu (SDGs), yanayolenga kutokomeza umaskini ifikapo mwaka 2030.

Mkutano huu unafanyika wakati ambapo taarifa zinaonyesha kasi ndogo ya kufikia malengo ya kuondoa umaskini duniani, kutokana na changamoto mbalimbali ikiwemo milipuko ya magonjwa, machafuko ya kisiasa, na kuanguka kwa bei ya mazao ambayo wananchi wengi wanayategemea kwa kipato.

#AzamTVUpdates
Mhariri | John Mbalamwezi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *