Nchini Sudan Kusini kukamatwa kwa Makamu wa kwanza wa rais Riek Machar siku ya Jumatano, kumeendelea kuzua hali ya wasiwasi katika nchi hiyo, huku wito wa utulivu ukiendelea kutolewa.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
Katika kipindi hiki, taarifa nyingi potofu na kauli zenye chuki, zinasambaa kwenye mitandao ya kijamii nchini humo, hali ambayo inaendelea kuzua mgawanyiko kati ya raia wa kawaida, hasa wafuasi wa rais Salva Kiir na Machar.
Siku ya Ijumaa, serikali ya Sudan Kusini, ilithibitisha kukamatwa na kuzuiwa kwa Machar nyumbani kwake, kwa madai kuwa alikuwa amepanga uasi dhidi ya uongozi wa rais Kiir.

Waziri wa habari na msemaji wa serikali Michael Makuei Lueth, alidokeza kuwa Makamu huyo wa kwanza rais, atachunguzwa na kuwataka raia wa nchi hiyo kusalia watulivu kipindi hiki.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, amesema anahofia hali ya nchi hiyo, na kuonya suluhu ya haraka kupatikana, ili kuepusha nchi hiyo kurejea kwenye vita.

Guteress amewataka viongozi wakuu wa nchi hiyo, kuweka silaha chini na kuwatanguliza raia wa Sudan Kusini.
Mjumbe maalum wa serikali ya Kenya na Jumuiya ya Afrika Mashariki na IGAD, Waziri Mkuu wa zamani Raila Odinga ametumwa kwenda kujaribu kutuliza na kuzuia uwekano wa kuzuka kwa vita.
Soma piaOdinga yuko Juba kusaidia katika upatanishi kati ya rais Kiir na makamu wake
Kwa sasa hali ya utulivu inaendelea kushuhudiwa jijini Juba, ambapo wakaazi wanaripotiwa kuendelea na shughuli zao kama kawaida, licha ya wasiwasi.