
Marekani imetangaza kupunguza kwa kiasi kikubwa bajeti kwa mipango ya maendeleo ya Marekani na misaada ya kigeni siku ya Jumatano, na kupunguzwa kwa hadi asilimia 90.
Imechapishwa:
Dakika 2
Matangazo ya kibiashara
Rais Donald Trump alitia saini agizo la utendaji mnamo Januari 20, aliporejea Ikulu ya White House, na kuagiza kusitishwa kwa msaada wa kigeni wa Marekani kwa siku 90, wakati wa mapitio kamili ya kutathmini ulinganifu wake na sera anazokusudia kufuata, haswa dhidi ya programu zinazohimiza uavyaji mimba, kupanga uzazi au kutetea utofauti na ushirikishwaji.
Lakini jaji wa shirikisho, aliyefikishiwa malalamiko na mashirika mawili yanayoleta pamoja makampuni, mashirika yasiyo ya kiserikali, na wanufaika wengine wa fedha za misaada za Marekani, alisitisha uamuzi huu wa kuzuia matumizi yaliyoidhinishwa na Baraza la Congress.
Kama sehemu ya utaratibu huu, kufuatia mapitio ya programu hizi zilizofanywa na huduma zake, Waziri wa Mambo ya Nje Marco Rubio, ambaye Shirika la Marekani la Misaada ya Kimaendeleo ya Kimataifa (USAID), ambalo lilitakiwa kvunjwa, aliamua kuondoa kabisa karibu 5,800 ya ufadhili uliotolewa ulimwenguni kote na shirika hili, na gharama iliyobaki ya dola bilioni 54, akibakiza zaidi ya 500 tu, kulingana na Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani. Zaidi ya hayo, kati ya zaidi ya ruzuku 9,100 zilizotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje, jumla ya dola bilioni 15.9, 4,100 – na gharama inayokadiriwa ya dola 4.4 bilioni – zimefutwa, msemaji wa Wizara ya mambo ya Nje ya Marekani amesema.
Ruzuku “muhimu” imedumishwa
USAID inaendelea kutoa ufadhili “muhimu” kama vile msaada wa chakula na matibabu kwa wagonjwa wa UKIMWI, kifua kikuu na malaria, pamoja na nchi kama vile Lebanoni, Haiti, Venezuela na Cuba, Wizara ya Mambo ya Nje imesema.
“Wizara ya Mambo ya Nje imesema leo imepunguza ufadhili wa dola 10,000 kutoka kwake na USAID, na kukata misaada ya nje ya Marekani,” InterAction, muungano wa zaidi ya mashirika 160 yasiyo ya kisetrikali, imesema katika taarifa. “Wanawake na watoto watateseka kwa njaa, chakula kitaozea kwenye maghala, watoto watazaliwa na VVU, miongoni mwa majanga mengine,” InterAction imeongeza, ikimsihi Bw. Rubio kutengua uamuzi ambao “hautaifanya Marekani kuwa salama, nguvu zaidi, au kuwa na ustawi zaidi.”
Mahakama pia iliamuru Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani kuanza tena malipo, yanayokadiriwa kuwa dola bilioni 1.5 hadi dola bilioni 2, kwa mamia ya mashirika ya misaada ya kimataifa ifikapo 5:59 usiku siku ya Jumatano (sawa na 5:59 Alfajiri Alhamisi saa za Ufaransa Alhamisi). Lakini Mahakama ya Juu yenye wahafidhina wengi, iliyopokea malalamiko kutoka utawala wa Trump, iliahirisha uamuzi huu ikitathmini uamuzi juu ya uhalali.
USAID, ambayo ilikuwa na wafanyakazi zaidi ya 10,000, ilitangaza Februari 23 kuwa inawaachisha kazi wafanyakazi wake 1,600 nchini Marekani na kuwaweka wengi wa wafanyakazi wake likizo ya utawala.
Hatu ya Donald Trump ya kuusitisha misaada imezua mshtuko na hisia ndani ya chombo hicho huru kilichoundwa na kitendo cha Bunge la Marekani mwaka 1961, ambacho kinasimamia bajeti ya kila mwaka ya dola bilioni 42.8, ikiwa ni asilimia 42 ya misaada ya kibinadamu inayotolewa duniani kote.
Rais huyo kutoka chama cha Republican aliahidi wakati wa kampeni yake kupunguza uzito wa serikali ya shirikisho na kupunguza matumizi, kabla ya kumteua mshirika wake bilionea Elon Musk kuongoza tume ya ufanisi ya serikali (Doge).