
Gazeti la Washington Post limeripoti kwamba kuna uwezekano wa Marekani kukabiliwa na tishio kubwa zaidi kuliko silaha za nyuklia katika siku za usoni, licha ya kwamba nchi hiyo ni mojawapo ya vinara katika kutafiti silaha za kibiolojia na na za vijidudu.
Gazeti la Washington Post limeandika kwamba katika zama hizi za baiolojia bandia, inawezekana katika siku za karibuni tukakabiliwa na maafa ya kibiolojia.
Ripoti hiyo ya utafiti ya Washington Post imesema kuwa, watafiti duniani kote wanashughulikia virusi ambavyo vinaua idadi kubwa zaidi kuliko Covid-19, jambo ambalo lina maana kwamba jinamizi la janga kubwa la kibaolojia haliko mbali.
Gazeti la Washington Post la Marekani limeandika kuwa kulingana na ripoti ya pamoja ya watafiti wa kibaolojia, Russia imefungua tena na kupanua eneo la kijeshi na maabara ambalo lilitumika wakati wa Vita Baridi kwa ajili ya kutengeneza silaha ya virusi inayosababisha ugonjwa wa ndui, Ebola na magonjwa mengine ya mlipuko.
Washington Post imeleeza kuwa, imeripotiwa kutoka China kwamba maafisa wakuu wa kijeshi wanatafiti manufaa ya vita vya kibaolojia. Limesema, maafisa hao wa China wanaelezea vita vya kibaolojia kuwa ni mbinu ya “nguvu na ya kistaarabu zaidi” ya maangamizi makubwa kuliko silaha za nyuklia.