Washindi 75 wa Tuzo ya Nobel watoa wito wa hatua ya kimataifa ya kukomesha mashariki mwa DRC

Washindi sabini na watano wa Tuzo ya Nobel wametia saini waraka siku ya Jumatano, Juni 4, wakiitaka jumuiya ya kimataifa kuchukua hatua kukomesha mateso ya raia watu wa Kongo. Waraka huo umeonekana kwenye Gazeti la kila siku la Le Monde. Wito huo ulitolewa kwa mpango wa Dk. Denis Mukwege, mwenyewe mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel mwaka 2018 kwa kazi yake mashariki mwa DRC kuwasaidia wanawake waathiriwa wa ubakaji, ambayo imekuwa silaha ya vita.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Idadi ya waliotia saini ni kubwa na orodha ni ya kuvutia. Washindi sabini na watano wa Tuzo za Nobel wa mataifa na taaluma mbalimbali, kuanzia kemia hadi fasihi, masuala ya dawa, na amani, kutoka kwa mwandishi wa Nigeria Wole Soyinka hadi David MacMillan, mwanakemia wa Uingereza, wametia saini waraka huo.

Kwa pamoja, wanashutumu “ukimya unaoendelea duniani” kuhusiana na uhalifu ulnofanyika mashariki mwa DRC. “Janga” ambalo limedumu kwa miongo mitatu ya “migogoro ya silaha, vita vya mara kwa mara, majanga ya kibinadamu, na ukiukwaji wa utaratibu wa haki za binadamu na sheria za kimataifa.” Na hali hii hutokea wakati tabia ya kutoajali au ya kutoadhibu huchochea migogoro na ukosefu wa hatua “muhimu” ya kuizuia.

Washindi 75 wa Tuzo ya Nobel kwa hiyo wanatoa wito wa kuandaliwa kwa mkutano wa kimataifa wa amani “kuweka mzozo huu uliosahaulika na kupuuzwa katika kilele cha ajenda ya jumuiya ya kimataifa.” Kuhusu vita vinavyoendelea, wanaikosoa jumuiya ya kimataifa kwa “kuvumilia” uwepo wa jeshi la Rwanda mashariki mwa nchi. “Uchokozi haramu,” kwa maneno yao, ambayo inaendelea licha ya Umoja wa Mataifa kupiga kura mwezi Februari juu ya azimio la kuitaka Rwanda kusitisha kuunga mkono M23. Watia saini wamelinganisha vali ya Mashariki mwa DRC na mzozo kati ya Ukraine na Urusi na kulaani hatua zinazoegemea upande mmoja.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *