
Wanasheria wawili wa kutoka Afrika, jaji wa Botswana Sanji Monageng na jaji wa Ghana Evelyn Ankumah, wamejiunga na kundi la washauri maalum wa mwendesha mashtaka wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu, ICC.
Imechapishwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
Uteuzi wa wanasheria hao wawili kutoka Afrika unakuja katika hali ya wasiwasi na wakati mwendesha mashtaka Karim Khan amekuwa, tangu mwisho wa mwezi wa Januari 2025, chini ya vikwazo kutoka kwa Marekani ambayo inapinga amri ya kukamatwa kwa Benjamin Netanyahu.
Wanasheria hao wawili wa Kiafrika kwa hiyo wanajiunga na mtandao wa washauri maalum. Uteuzi huu unafanya idadi ya Waafrika kufikia wanne kati ya jumla ya washauri 16. Tayari wamejumuishwa Mohamed Othman, mwenyekiti wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kutafuta ukweli kuhusu Sudan, na Adama Dieng, mjumbe maalumu wa zamani wa Umoja wa Mataifa anayeshughulika na kuzuia mauaji ya watu wengi, ambaye sasa anahudumu katika Umoja wa Afrika.
Mkutano mnamo Julai 2025
Jaji Sanji Monageng amekuwa Kamishna Mkuu wa Botswana nchini Afrika Kusini tangu 2022. Hapo awali, alikuwa jaji katika ICC kwa miaka tisa. Mwanasheria Evelyn Ankumah ndiye mwanzilishi wa Africa Legal Aid, chombo cha kufikiri juu ya haki ya kimataifa ambacho kinatetea hasa marekebisho ya uhalifu wa “uchokozi”, kwa sababu maandishi ya sasa ya Mahakama hayaruhusu kufunguliwa mashitaka madhubuti kwa wahusika.
Swali ambalo Bunge la nchi wanachama 125 wa Mahakama lazima liamue katika mkutano uliopangwa kufanyika mwezi Julai 2025 huko New York.