Wasaheli milioni 29 wanahitaji msaada wa haraka wa kibinadamu kwa ufadhili usio na uhakika

Takriban watu milioni 29 wanahitaji msaada wa dharura wa kibinadamu na ulinzi katika ukanda wa Sahel. Hii ni kwa mujibu wa ripoti iliyochapishwa wiki hii na Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu (OCHA). Utafiti huo unahusu Burkina Faso, Chad, Mali, Niger, pamoja na kaskazini ya mbali ya Cameroon na kaskazini mashariki mwa Nigeria. Shirika hilo linatoa wito kwa wafadhili, likionya kwamba bila ufadhili unaohitajika, maisha ya mamilioni ya watu yatakuwa hatarini.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Kulingana na OCHA, takwimu zimeongezeka kwa 6% na 20% mtawalia tangu mwanzoni mwa mwaka 2024: Sahel sasa ina wakimbizi milioni 2 na wakimbizi wa ndani milioni 6. kukimbia huku kwa watu kunahusishwa na migogoro mbalimbali iliyoingiliana: ukosefu wa usalama, umaskini, kukosekana kwa utulivu wa kisiasa, na matokeo ya mabadiliko ya tabianchi, miongoni mwa mengine.

Kati ya mwezi Juni na mwezi , OCHA inakadiria kuwa zaidi ya watu milioni 12 watakabiliwa na uhaba wa chakula katika eneo la Sahel.

Mwaka jana, matukio mengi ya usalama yalitokea katika Sahel ya Kati na Bonde la Ziwa Chad. Matokeo hayo yalisababisha karibu vifo 17,000 na kusababisha kufungwa kwa takriban vituo 1,000 vya afya na karibu shule 10,000-zaidi ya nusu yao ziko Burkina Faso.

Matokeo ya migogoro ya Sahel yanazidi mipaka ya eneo hilo, OCHA inaonya, na kusambaa hadi katika nchi za pwani za Afrika Magharibi, ambazo mikoa yake ya kaskazini inahifadhi wakimbizi 159,000.

Hata hivyo, fedha zinakosekana kutatua changamoto hizi. Zaidi ya dola bilioni 4 zinahitajika ili kukidhi mahitaji ya dharura ya kibinadamu ya Wasahel milioni kadhaa. Mkuu wa ofisi ya kikanda ya OCHA anakumbusha kuwa si kuhusu kusawazisha ripoti, bali ni kuokoa maisha ya binadamu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *