Waridi wa BBC: ‘Saratani si hukumu ya kifo’

Kabla hajakatwa mguu, Annah hakupenda kupigwa picha. Lakini baada ya safari yake ya saratani, aliamua kutumia mitandao ya kijamii kuhamasisha wengine, kupinga unyanyapaa dhidi ya watu wenye ulemavu na kuelimisha jamii kuhusu saratani.