
Kundi la Mamluki wa Tigray kwa jina Army 70 lenye uhusiano na wapiganaji wa TPLF kaskazini mwa Ethiopia ,sasa linatuhumiwa kupigana pamoja na vikosi vya Sudan katika mapigano yanayoendelea.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Vyanzo kutoka eneo hilo vinasema mamluki hao wa Army 70 wametumwa mashariki mwa Sudan kwa msaada wa Tigray People’s Liberation Front (TPLF), kusaidia jeshi la Sudan katika mapambano na wanamigambo wa RSF.
Inadaiwa kuwa kila mamluki waliotumwa kuwasaidia wanajeshi chini ya Jenerali Abdel Fattah al Burhan, walikuwa wanalipwa Dola 200 kila mmoja na mawakala ndani la TPLF walilipwa hadi Dola Elfu Moja.
Mpango huo wa Army 70, ulijumuisha mipangilio ya siri, kuhamishwa pesa bila mamlaka za Ethiopia kufahamu.
Hii inaibua wasi wasi ya mzozo wa Sudan kuhusisha mataifa mengine.
Kiongozi wa RSF Mohammed Dagala, ameishtumu TPLF kwa kufadhili na kuwapa mafunzo wapiganaji wanaowasaidia wanajeshi wa Sudan na kulaani nchi za kigeni kuchochea mzozo wa Sudan.
Umoja wa Afrika na muungano wa kimaendelea wa serikali IGAD, bado zimesalia kimya kuhusu tuhuma hizo ila kuna shinikizo la kuchungwa kwa madai hayo.