Wapalestina wa Ghaza: Trump ni kichaa, hajui chochote kuhusu ardhi yake mtu, sharafu wala Palestina

Wapalestina wa Ukanda wa Ghaza wameubeza na kuukebehi mpango wa Rais wa Marekani wa kuwataka wahame moja kwa moja katika ardhi yao hiyo ya Palestina ili kupisha ujenzi wa kuigeuza Ghaza eneo la burudani watakaloishi ndani yake watu wa kila pembe ya dunia.