Wapalestina 79 waliotolewa kwenye jela za Israel walazimika kwenda kuishi uhamishoni nje ya nchi yao

Afisa wa vyombo vya habari katika ofisi ya Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS inayoshuughulikia masuala ya mateka Wapalestina amethibitisha kuwa mateka 79 wa Kipalestina walioachiliwa huru na utawala wa Kizayuni wa Israel kama sehemu ya makubaliano ya kusitisha mapigano na kubadilishana mateka Ghaza wamewasili Cairo baada ya kufukuzwa na utawala huo na kuhamishiwa nchini Misri.