Wapalestina 369 mkabala wa Waisraeli 3 wanaachiwa leo katika duru ya sita ya kubadilishana mateka

Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS imetaja majina ya mateka watatu wa Israel wenye uraia pacha ambao wanatazamiwa kuachiliwa leo kama sehemu ya duru ya sita ya mabadilishano ya mateka chini ya awamu ya kwanza ya makubaliano ya kusitisha vita katika Ukanda wa Ghaza.