Wanasheria Tunisia: Kesi ya Instalingo ni njama ya Kisiasa ya kuwamaliza wapinzani wa serikali

Maamuzi yaliyotolewa na mahakama ya Tunisia katika kesi inayojulikama kama “Instalingo” yanaendelea kuibua hisia hasi kutoka kwa mawakili, wanaharakati wa kutetea haki za binadamu na timu ya utetezi kwa washtakiwa, ambao wanayataja maamuzi hayo kuwa yasiyo na mantiki wala msingi wa kisheria, na kwamba lengo lake ni kuwafutilia mbali wapinzani wa kisiasa wa serikali ya Tunis.