Wanajeshi wa RSF wa Sudani na washirika wake watia saini mkataba wa kuunda serikali pinzani

Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF° nchini Sudani na washirika wao siku ya Jumapili wametia saini hati ambayo inafungua njia ya kuanzishwa kwa serikali pinzani, huku jeshi la Sudani likipiga hatua hivi karibuni dhidi ya makundi hasimu.

Imechapishwa:

Dakika 1

Matangazo ya kibiashara

Hafla ya utiaji saini huo ilifanyika katika faragha katika mji mkuu wa Kenya, Nairobi, baada ya mkutano wa uliorushwa na vyombo vya habari wiki iliyopita katika jengo la serikali ya Kenya kulaaniwa na wizara ya mambo ya nje mjini Khartoum.

Waliotia saini walisema wataanzisha serikali ya “amani na umoja” licha ya wasiwasi kutoka kwa mashirika ya haki za binadamu na jumuiya ya kimataifa, ambayo imeshutumu RSF kwa kufanya ukatili na mauaji ya halaiki tangu ilipoanza kupambana na jeshi la Sudani mwezi Aprili 2023.

Vita nchini Sudani vimewauwa zaidi ya watu 24,000 na kusababisha zaidi ya watu milioni 14 – karibu 30% ya watu – kutoroka makazi yao, kulingana na Umoja wa Mataifa. Takriban raia milioni 3.2 wa Sudani wamekimbilia nchi jirani.

Umoja wa Mataifa wiki iliyopita ulisema kuwa katika kipindi chote cha mwaka 2024, ofisi yake ya haki za binadamu ilirekodi zaidi ya mauaji ya raia 4,200, na kuongeza kuwa idadi hiyo inaweza kuwa kubwa zaidi.

Jeshi la Sudani limepata nguvu katika mzozo huo huku RSF ikikabiliwa na mapigo mengi, ikiwa ni pamoja na kupoteza udhibiti wa mji wa Wad Medani, mji mkuu wa jimbo la Gezira, na maeneo mengine katika jimbo hilo. Jeshi la Sudani pia lilipata udhibiti wa kiwanda kikubwa zaidi cha kusafisha mafuta nchini humo.

RSF inaonekana kupoteza udhibiti wa eneo la Greater Khartoum na miji ya Omdurman na Khartoum Bahri.